DJ akana kugusa makalio ya Taylor Swift
DJ wa zamani wa redio David Mueller
amekana madai yaliyotolewa na mwanamuziki Taylor Swift kwamba
alimdhalilisha wakati alipokutana na mashabiki wake.
Ni mara ya kwanza kwa Bwana Mueller kuzungumzia kuhusu kile kilichotokea kabla ya tamasha la Detroit mwaka 2013.Taylor anamshitaka kwa kumdhalilisha na kumtia aibu katika tukio hilo analosema lilimuacha "lilimshitua na kumfanya ajitenge na watu".
ADJ wa zamani wa redio David Mueller amekana madai yaliyotolewa na mwanamuziki Taylor Swift kwamba alimdhalilisha wakati wa wakati alipokutana na mashabiki wake.
DJ huyo wa zamani alifutwa kazi katika kituo cha kaunti cha muziki cha Colorado cobaada ya tukio hilo na sasa amezungumzia kuhusu mashtaka ya kisheria dhidi ya kipindi cha kituo cha redio cha Detroit, cha- Mojo In The Morning.
Tovuti ya Marekani TMZ umesambaza picha kutoka kwenye kipindi hicho kilichojulikana kama -meet and greet , ambazo David anasema hazikumuonyesha akimguza Taylor.
"Najaribu kupitisha mkono wangu wa kulia nyuma ya Taylor kwasababu Shannon (mpenzi wake wa kike) alikuwa upande mwingine wa Taylor," alielezea David , alipokuwa akijadili kuhusu picha hiyo.
''Mkono wangu ulikuwa kwenye mkanda wangu tu ama ndani ya mifuko ya suruari yangu ."
"kwa hiyo mkono wangu mwingine ulikuwa nyuma ya Taylor. "ulikwenda nyuma yake na mkono wake ukaenda nyuma yangu."
Mikono yetu ilipishana ,hicho ndicho ninachokikumbuka.
Nyaraka za kisheria zilizosambazwa kwenye mtandao wa internet mapema mwezi Novemba ambazo ziliripotiwa kuonyesha waraka wa maswali ambayo mahakama iliwahoji mawakili wa David na Taylor, Taylor alitoa shutuma zake.
"alipitisha mkono wake chini ya nguo yangu na kushika makalio yangu yaliyokuwa tupu ," alisema Taylor.
Leave a Comment