Sasa unaweza kupima HIV kwa kifimbo hiki cha USB

Una wasiwasi kuwa mchepuko uliolala nao jana unaweza ukawa hauko salama na unataka kupima ngoma? Hutohitaji kwenda hospitali kujua afya yako, kifimbo hiki cha USB kinaweza kukupa majibu iwapo umeukwaa ama uko fit!
3a3ab30e00000578-0-image-a-23_1478771163390
Wanasayansi wa Uingereza wamevumbua njia mpya ya kupima HIV ambayo itahitaji tu kuchomeka kifaa kwenye kompyuta kama unavyochomeka USB Flash. Watafiti wanadai kuwa kifaa hicho kinaweza kubaini virusi kwenye tone la damu na kutoa majibu yanayoweza kusomwa kwenye laptop.
3a3a870d00000578-0-uk_scientists_have_developed_a_usb_test_pictured_which_can_detec-a-22_1478771155567
Kifaa hicho kinaweza kutoa majibu ndani ya dakika 30. kimetengenezwa na timu ya Imperial College London na kampuni ya DNA Electronics.
3a3a870600000578-3923136-the_hope_is_that_quick_and_effective_diagnostic_tests_like_the_u-a-25_1478772230230

Hakuna maoni

GESHACK MEDIA & ENTERTAINMENT.0754 981 696. Inaendeshwa na Blogger.